Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na mabalozi wa heshima watakaoiwakilisha Tanzania katika
majimbo mbalimbali nchini Marekani wakati wa hafla ya kuwapa hati za
utambulisho zilizofanyika katika ubalozi wa Tanzania jijini Washington Marekani.
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa maslahi ya makampuni ya Marekani yanayotaka kuwekeza katika Tanzania hayataathiriwa na kuwepo kwa China katika uchumi wa Tanzania kwa sababu China siyo moja ya wawekezaji wakuu katika uchumi wa Tanzania kwa sasa.
Amesema
kuwa miongoni mwa wawekezaji wakuu wa uchumi wa Tanzania, China inashikilia
nafasi ya 10 huku Uingereza ikiwa inaongoza katika kuwekeza katika Tanzania.
Aidha, Rais Kikwete
amesema kuwa China ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa misaada ya maendeleo
kwa Tanzania lakini siyo katika makampuni ya nchi hiyo kuwekeza katika uchumi
wa Tanzania na hivyo nchi hiyo haiwezi kuwa tishio kwa uwekezaji wa makampuni ya
Marekani.
Ametoa
ufafanuzi huo wakati alipokutana katika
mkutano wa kikazi na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Mahusiano ya Nje na Bajeti
ya Miradi ya Maendeleo ya Bunge la Marekani mjini Washington, D.C., pamoja na
baadhi ya wajumbe wa kamati yake.
Katika mkutano huo,
Rais Kikwete aliulizwa jinsi gani fedha ya Jamhuri ya Watu wa China katika
uchumi wa Tanzania inavyoathiri uwekezaji wa makampuni ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment