BAADHI ya wabunge wa upinzani
nchini Kenya wameondoka bungeni wakati mjadala mkali ukiendelea kuhusu kuunga
mkono au kupinga nchi hiyo kujiondoa kutoka katika mahakama ya kimataifa ya
ICC.
Wabunge hao wameondoka bungeni
baada ya kusema kuwa kamwe hawataungana na upande wa serikali kuunga mkono hoja
hii ya kujiondoa kutoka katika mahak
ama ya ICC. Ni kutokana na kuwa
kwamba upinzani una idadi ndogo zaidi ya wabunge bungeni.
Naibu kiranja wa wabunge walio
wachache bungeni Jakoyo Midiwo, alisema kuwa wabunge wa upande wa serikali
wanaotetea hoja hii ya kujondoa Hague watakuja kujuta.
Mjadala huu unatokana na hatua ya
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kukabiliwa na kesi za uhalifu
dhidi ya binadamu katika mahakama hiyo wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi
mkuu mwaka 2007-2008.
Hatua hii ya wabunge inakuja
zaidi ya wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya naibu Rais wa Kenya
Williiam Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.
Ruto anakabiliwa na mashtaka ya
uhalifu dhidi ya binadamu.
Rais Uhuru Kenyatta pia
anatarajiwa kufika katika mahakama hiyo mwezi Novemba kwa kesi dhidi yake.
Wawili hao wanashtakiwa kwa
kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2007.
Msemaji wa ICC ameambia BBC kuwa
kesi hiyo itaendelea hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma
uliopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
Bwana Fadi El Abdallah, alisema
kuwa itachukua karibu mwaka mmoja kwa mchakato wa nchi yoyote ile kujiondoa
kutoka katika mahakama ya ICC na hii bila shaka inaathiri tu kesi zilizokuwa
mbele ya mahakama hiyo kwa wakati huo.
Hii ni hatua ya dharura
inayochukua serikali kujitoa katika Mkataba wa Roma wa mahakama hiyo
ulioidhinishwa na Umoja wa mataifa mnamo tarehe 17 July, mwaka1998.
Kenya inataka kutoa mfano wa kuwa
nchi ya kwanza Afrika kuchukua hatua hiyo licha ya kwamba uamuzi huu
hautoathiri kwa namna yoyote kesi zinazoendelea sasa katika mahakama ya ICC.
Mahakama hiyo ya kimataifa
imesema kwamba kesi hizo zitaendelea hata iwapo Kenya itajitoa.
Imesema itaichukua Kenya kiasi ya
mwaka mmoja kabla ya kukubaliwa ombi hilo la kutaka kujiondoa katika mkataba wa
Roma na hilo litaathiri tu kesi zitakazozuka baada ya muda huo.
Haya yanajiri wakati makamu wa
rais William Ruto anatarajiwa kuondoka Kenya kueleka Hague Uholanzi wiki ijayo
kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadaamu katika mahakama hiyo ya
ICC, kesi inayoanza tarehe 10 mwezi huu.
Wote wameshtakiwa kwa kuhusika katika ghasia
zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.Kesi dhidi ya rais Uhuru
Kenyatta inatarajiwa kuanza tarehe 12 mwezi Novemba. BBC
0 comments:
Post a Comment