MATUKIO ya uvunjifu wa maadili kwenye shule
mbalimbali hapa nchini yameendelea kushamiri baada ya wanafunzi wanne wa Shule
ya Msingi lulanzi wilayani kibaha mkoani pwani kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa
darasa la pili na kumsababishia maumivu yaliyopelekea hadi kulazwa Hospitali ya
Tumbi kwa matibabu.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi jana babu wa mtoto huyo, Jacob Mrope alisema tukio hilo lilitokea Septemba
2 saa 6 mchana ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima alikuwa akitoka shuleni huku
akiwa na wenzake wawili wa kike, walikimbizwa na watuhumiwa hao ambapo yeye
alishindwa kukimbia kutokana na kuumia mguu na kujikuta akibakwa.
Mrope alisema kuwa wanafunzi
wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba
mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza
kupata msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao.
"Wenzake waliokuwa nao
walitoa taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na
kumkuta akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka
ndipo alimchukua na kumpeleka shuleni kutoa taarifa," alisema Mrope.
Kwa upande wake dada yake Lwiza
alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao alikuwa nao
wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa
ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu, wamkokota mwenzao hadi nyumba
iliyojirani na kumjulisha.
"Alikuwa kwenye hali mbaya
kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na
mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na
wenzake watatu," alisema Lwiza.
Lwiza alisema kuwa baada ya kuona
hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za
kisheria ambapo walikwenda Serikali ya mtaa kisha kwenda polisi na baadaye Hospitali
ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa bado
kalazwa na hali yake inasemekana kuwa ni mbaya.
Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya
Lulanzi, Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema
lolote kwani suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na
watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.
"Ni kweli tukio hili
limetokea lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje
ya shule na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa
kurudi nyumbani mara baada ya masomo kwisha," alisema Bilali.
Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa
mtaa wa Lulanzi, Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushangazwa
na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule
hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi
wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa
wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na
tukio hilo.
Sina habari. blogsport. com.
0 comments:
Post a Comment