Mhadhiri mmoja wa kidini nchini Saudi Arabia amehukumiwa kifungo cha
miaka minane jela na kuchapwa viboko 800 kwa kosa la kumnajisi bintiye mdogo wa
miaka mitano na kumtesa hadi kufariki dunia.
Mahakama ya Saudi Arabia Jumatatu
hii ilimuamuru Fayhan al Ghamdi kumlipa mke wake wa zamani yaani mama wa binti
huyo fedha za diya ya damu dola za Kimarekani 270,000.
Mke wa pili wa mahdhiri
huyo aliyekutwa na hatia ambaye naye ameshtakiwa kwa kushiriki kwenye jinai
hiyo amehukumiwa kifungo cha miezi kumi jela na viboko 150.
Binti huyo wa
Saudia aliyekuwa na umri wa miaka mitano alilazwa hospitali mwezi Disemba mwaka
juzi akiwa na majeraha kadhaa, michubuko, majeraha ya kuungua moto na kupasuka
fuvu la kichwa.
Wanaharakati nchini Saudi Arabia na wa nchi za nje wamelaani
vikali jinai hiyo iliyofanywa na baba huyo kwa bintiye na kuitaja adhabu
iliyotolewa na mahakama ya nchi hiyo kwa mtenda jinai huyo kuwa ya kiwango cha
chini mno.
Wanaharakati hao wamesema mtenda jinai huyo alipaswa kufungwa jela
maisha au kunyongwa ili iwe mfano kwa wengine.
0 comments:
Post a Comment