Kwa sasa ufoo Saro
amehamishiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea hospitali ya
Tumbi, na taarifa za awali inadaiwa
amejeruhiwa kwa risasi kwenye bega na tumboni.
Taaarifa ambazo
hazijathibitishwa inasemekana kulikua na ugomvi kati ya Ufoo na Mpenzi wake na
baada ya kushindwa kuelewana waliamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo kwa ajili
ya usuluhishi.
Inadaiwa kuwa mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe kwamba
anamtetea mwanae na ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake Ufoo Risasi ya
kichwa na kumuua papo hapo, na kisha akampiga Ufoo Saro risasi mbili moja ya
tumboni na nyingine ya begani akidhani amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha
akajipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
Jeshi la polisi bado
linaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha tukio hilo na limehaidi kutoa taarifa
kamili wakati wowote.
Miili ya Marehemu mama
yake Ufoo Saro pamoja na mpenzi wake Ufoo saro imehifadhiwa kwenye hospitali ya
Taifa Muhimbili.


0 comments:
Post a Comment