Mwl Julius Kambarege.
Na. AUGUSTINE MGENDI,
BUTIAMA.
Zaidi ya Vijana 400
kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wanatarajiwa kushiriki katika Kongamano la
kuadhimisha Miaka 14 tangu kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarege
Nyerere katika wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
Kongamano hilo
litakalofanyika Oktoba 14 katika eneo la Mwitongo wilaya ya Butiama mkoani Mara
likiwa limeandaliwa na Umoja wa Vijana
Mkoa wa Mara,ofisi ya wilaya hiyo na Makumbusho ya hayati baba wa Taifa ambapo
litakuwa na mada kuu mbili.
Mkuu wa wilaya ya
Butiama Bi Angelina Mabula amesema kuwa lengo la kongamano hilo kuwakumbusha
Vijana juu ya falsafa za hayati baba wa Taifa ambapo Mkurugenzi mtendaji
wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph
Butiku na Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono watatoa Mada kuhusu
Maendeleo vijijini na ajira kwa Vijana pamoja na miiko ya Viongozi.
Angelina Mabula
Aidha baadhi ya Wazee
wa eneo hilo la Butiama Mkoani hapa wameelezea mambo mbalimbali ambayo
yameonekana miaka kumi na nne tangu kifo cha hayati baba wa Taifa Mwl Julius
Kambarage Nyerere.
Kongamano hilo litakuwa
la Kwanza kufanyika wilayani hapa likiwa linahusisha Vijana Mbalimbali kutoka
Tanzania katika kukumbushwa falsafa za hayati Mwalimu Julius Kambarege Nyerere
ambapo Mkuu wa wilaya hiyo amesema litakuwa likifanyika kila Mwaka.");



0 comments:
Post a Comment