Mhe. Benjamini William Mkapa.
Na.Benedict Liwenga, Dar es Salaam.
RAIS Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa amezindua rasmi
Kampeni ya “Tusome Tanzania (Let’s
read Tanzania Campaign) iliyoandaliwa na wadau mbalimbali nchini wenye
lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kusoma
vitabu mbalimbali.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Mkapa ameipongeza kamati ya wadau
waandaaji wa kampeni hiyo kwa kujitoa kwao katika kuhakikisha kuwa watoto wa
shule ambao ndiyo taifa la kesho wanapata kujionea wenyewe na anatumaini kuwa
watahamasika kupenda kujisomea kwa manufaa ya maisha yao.
“Tabia ya kusoma inamjenga mtu kifikra na kumpa mtu mtazamo”.
Alisema Mhe. Mkapa.
Mhe. Mkapa ameongeza kuwa kwa kuwa elimu haina mwisho, kusoma ni
namna ya kujielimisha siku hadi siku na kufungua mambo mapya yanayoipa akili
changamoto, hivyo amewasisitizia vijana wajijengee utamaduni wa kusoma hasa
vitabu vya kiswahili na Kiingereza.
“Someni kazi za Shaabani Robert mwandishi mkongwe wa
Tanzania, someni kazi za Mariam Abdallah, Ngugi wa Thio’ngo , Chinua
Achebe, Ole Soyinka na .” Alisema Mhe. Mkapa.
Aidha, Mhe. Mkapa ametoarai kwa wadau waandalizi wa kampeni ya “Let’s read Tanzania Campaign” kuwa
zoezi hilo lisiishie hapo bali liwe endelevu na kuwafikia watu wengi na haswa
vijana, pia amesisitiza kuwa mtandao wa vitabu uhakikishe vitabu hivi vinafika
hadi kwenye shule za vijijini na amehamisisha juu ya ujenzi wa Maktaba na
kusaidia kuboresha watoto wetu.
Let’s
read Tanzania Campaign ni kampeni iliyoandaliwa na vijana kutoka hasasi
mbalimbali lenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea
utamaduni wa kupenda kusoma vitabu kwa ajili ya kuongeza fikra za vijana na
kuwasaidia katika maisha yao.


0 comments:
Post a Comment