NYALLA,
NYAULINGO, NYENZI WASHINDA RUFANI
Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imewarejesha warufani wote watatu katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Kamati
mpya ya Utendaji ya TFF utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Samwel
Nyalla, Ayubu Nyaulingo na Ayoub Nyenzi walikata rufani mbele ya Kamati hiyo
inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda kupinga uamuzi
wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwaondoa katika uchaguzi huo ambapo wote
wanagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda mbalimbali.
Akisoma
uamuzi wao leo (Oktoba 11 mwaka huu) mbele ya Waandishi wa Habari kwenye ofisi
za TFF, Jaji Luanda amesema baada ya kusikiliza hoja za Mrufani Nyalla
walipitia Kanuni za Uchaguzi za TFF na kugundua yafuatayo;
Ibara
ya 10(3) imeweka masharti makuu mawili ya ujazaji wa fomu za kugombea uongozi.
Fomu hiyo ni lazima iwe na saini ya mgombea na ni lazima ithibitishwe na
viongozi wa shirikisho.
Kamati
imepitia Kanuni za Uchaguzi haijaona sehemu fomu hiyo ya uongozi imeambatanishwa
ili kuifanya kuwa Kanuni ya Uchaguzi. Ni maoni ya Kamati kuwa ni vizuri fomu za
kugombea zikawa ni sehemu ya Kanuni za Uchaguzi.
Kwa
vile Kanuni za Uchaguzi za TFF za 2013 pia hazijaainisha nini adhabu kwa
mgombea aliyekosea kujaza Fomu namba 1 ya kugombea uongozi, Kamati inaona
itakuwa si haki kumnyima mgombea nafasi ya kushiriki katika uchaguzi kwa vile
tu fomu yake haijajazwa vipengele vyote.
Nyalla
aliondolewa kwenye uchaguzi na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa maelezo kuwa si
mtu makini anayeweza kutekeleza majukumu yake kikamilifu baada ya kushindwa
kujaza Fomu namba 1 kipengele cha 15 kinachohusu malengo ya mgombea uongozi.
Kwa
upande wa Nyaulingo ambaye aliondolewa kwa kukosa uzoefu uliothibitika
kulingana na Ibara ya 29(3) ya Katiba ya TFF na Kanuni ya 9(3) ya Kanuni za
Uchaguzi za TFF, Kamati ya Rufani imeamua ifuatavyo;
Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi imepokea sababu za rufani na imepata fursa ya kusikiliza
hoja na maelezo kutoka kwa Mrufani juu ya sababu zake alizozitoa kupinga uamuzi
wa Kamati ya Uchaguzi.
Mrufani
alifafanua historia yake katika masuala ya michezo kuanzia alipokuwa anasema
Chuo Kikuu kuanzia 2005-2009 na pia ushiriki wake kama mchezaji wa Rukwa United
iliyowahi kushiriki Ligi ya Mkoa wa Rukwa na ligi nyingine za kitaifa.
Kwa
kusoma maana ya ‘Familia ya TFF’ iliyoko kwenye utangulizi wa Katiba ya TFF,
pamoja na Ibara ya 29(3) na 29(6) ya Katiba hiyo, Kamati imejiridhisha kuwa
Mrufani ana sifa za kugombea uongozi wa Shirikisho na amekidhi kigezo cha sifa
za ugombea.
Ameshiriki
kwenye mchezo wa mpira wa miguu kama mchezaji na mtawala, hivyo kutimiza kigezo
kilichohitajika cha ushiriki katika uongozi na utawala wa mchezo wa mpira wa
miguu kwa muda usiopungua miaka mitano.
Kwa
kuzingatia hayo, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inaruhusu rufani ya Mrufani.
Uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi umetenguliwa na Mrufani anapewa nafasi ya
kushiriki katika uchaguzi.
Kuhusu
Ayubu Nyenzi aliyeondolewa kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) ya
Katiba ya TFF na Kanuni ya 9(3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF, na pia kushindwa
kuthibitisha uraia wake mbele ya Kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Rufani katika
uamuzi wake imesema;
Imepokea
sababu za rufani na imepata fursa ya kusikiliza hoja na maelezo kutoka kwa
Mrufani juu ya sababu zake alizozitoa kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi.
Baada
ya uchambuzi wa kina, Kamati imeona kuwa kulingana na maelezo yaliyotolewa na
Mrufani na viambatanisho vilivyowasilishwa, Kamati haina shaka kuhusu uraia
wake. Uthibitisho wa uraia unapaswa kufanywa kwa umakini na taasisi yenye
mamlaka ya kiserikali kufanya hivyo.
Kamati
pia imejiridhisha kupitia Fomu namba 1 iliyojazwa na kusainiwa na Mrufani kuwa
kuanzia mwaka 2004 mpaka 2010, Nyenzi ameshika nyadhifa za utawala wa mpira wa
miguu na hasa katika klabu ya Yanga, uzoefu unaomfanya kuwa na sifa ya kugombea
nafasi ya uongozi katika TFF kulingana na Ibara ya 29(3) ikisomwa pamoja na
Ibara ya 29(6).
Kwa
kuzingatia hayo, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inaruhusu rufani ya Mrufani.
Uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi umetenguliwa na Mrufani atashiriki katika uchaguzi
wa TFF kwa nafasi anayogombea.
Wakati
huo huo, Kamati ya Rufani ya Maadili ya TFF inakutana keshokutwa (Oktoba
13 mwaka huu), kufanyia mapitio (revision) ya uamuzi wa Kamati ya Maadili kwa
waombaji uongozi wanane kama ilivyoombwa na Sekretarieti ili kutoa mwongozo wa
utekelezaji wa uamuzi huo.
VITAMBULISHO
KURIPOTI KOMBE LA DUNIA
Maombi
ya vitambulisho kwa waandishi wa habari (Accreditation) wanaotaka kuripoti
Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil kwa Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) yataanza kupokelewa kwa mtandao Desemba 7
mwaka huu kupitia akaunti ya FIFA Media Channel.
Mwisho
wa kupokea maombi hayo itakuwa Januari 31 mwakani, hivyo kwa waandishi
wanaotaka kupata vitambulisho hivyo ni lazima wawe na akaunti ya FIFA Media
Channel pamoja na utambulisho wa mtumiaji wa akaunti hiyo (user ID).
Kwa
mujibu wa FIFA, kila nchi itapewa idadi maalumu ya nafasi kwa waandishi
(waandishi wa kawaida pamoja na wapiga picha) baada ya mechi za mchujo za Kombe
la Dunia kumalizika ambapo vigezo mbalimbali vitazingatiwa ikiwemo nchi kufuzu
kwa fainali hizo.
Hivyo,
nchi ambayo itakuwa imefuzu itakuwa na nafasi zaidi kulinganisha na zile ambazo
hazitakuwa na timu katika fainali hizo za Brazil.
Mgawanyo
wa nafasi zitakazotolewa kwa Tanzania utapangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA) kulingana na maombi yatakayokuwa yamewasilishwa FIFA kupitia
FIFA Media Channel.
TFF
inatoa mwito kwa waandishi wa habari za mpira wa miguu ambao hawana akaunti
FIFA Media Channel kuhakikisha wanakuwa nayo mapema ili waweze kutuma maombi
yao.
SIMBA
YAIVAA PRISONS, YANGA MGENI BUKOBA VPL
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inakamilisha raundi ya
nane kesho (Oktoba 12 mwaka huu) kwa mechi tatu zitakazochezwa Dar es Salaam na
Bukoba mkoani Kagera.
Simba
ina fursa ya kuendelea kukamata usukani wa ligi hiyo iwapo itaishinda Tanzania
Prisons ya Mbeya katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia saa 10 jioni. Tanzania Prisons inayofundishwa na Jumanne Chale inashika
nafasi ya kumi na moja katika msimamo wa ligi hiyo.
Ili
iendelee kupanda katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo iliyoanza
Agosti 24 mwaka huu, Tanzania Prisons ambayo katika mechi yake iliyopita
ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo Shooting inalazimika
kuifunga Simba.
Licha
ya sare ya bao 1-1 katika mechi yake iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting, Simba
inayoongoza kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Azam na Mbeya City matokeo
mazuri katika mchezo huo ni muhimu kwao kama ilivyo kwa wapinzani wao Tanzania
Prisons.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000
ambapo tiketi zitauzwa uwanjani kwenye magari maalumu kuanzia saa 4 kamili
asubuhi.
Mabingwa
watetezi Yanga wao watakuwa mjini Bukoba kwenye Uwanja wa Kaitaba kuwakabili
wenyeji Kagera Sugar wanaofundishwa na Mganda Jackson Mayanja akisaidiwa na
Mrage Kabage.
Kagera
ambayo inapishana na Yanga kwa tofauti ya pointi moja ilipoteza mechi iliyopita
dhidi ya JKT Ruvu baada ya kulala kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Wakati Yanga ikiwa katika nafasi ya nne kwa pointi 12, Kagera Sugar ni ya sita
kwa pointi kumi na moja.
Iwapo
Kocha Ernst Brandts atawaongoza vijana wake wa Yanga kuibuka na ushindi katika
mechi hiyo na Simba kufanya vibaya kwenye mechi dhidi ya Tanzania Prisons
huenda akakamata uongozi wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 14.
Mwamuzi
Zakaria Jacob wa Pwani ndiye atakayechezesha mechi kati ya Ashanti United na
Coastal Union itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es
Salaam.
Raundi
ya tisa ya ligi hiyo inaanza keshokutwa Jumapili (Oktoba 13 mwaka huu) kwa
mechi kati ya Ruvu Shooting na Rhino Rangers (Mabatini, Mlandizi), Mgambo
Shooting na Mbeya City (Mkwakwani, Tanga), Azam na JKT Ruvu (Azam Complex, Dar
es Salaam) na Mtibwa Sugar na Oljoro JKT (Manungu, Turiani).
Mechi
zitakazooneshwa moja kwa moja (live) na Azam TV kupitia TBC1 wikiendi hii ni
kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na ile kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Jumapili
kwenye Uwanja wa Azam Complex.
FDL
KUTIMUA VUMBI WIKIENDI HII
Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kwa makundi yote matatu inaendelea wikiendi hii ambapo
kundi B litakuwa na mechi moja tu kati ya Lipuli na Mlale JKT itakayochezwa
kesho (Oktoba 12 mwaka huu) katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Transit
Camp itakwaruzana na Tessema katika Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi wakati
Polisi Dar itaumana na African Lyon kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar
es Salaam katika mechi za kundi A zitakazochezwa kesho (Oktoba 12 mwaka huu).
Mechi
nyingine ya kundi hilo itachezwa keshokutwa (Oktoba 13 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa kuzikutanisha Friends Rangers na
Villa Squad.
Timu
zote nane za kundi C zinashuka viwanjani kesho (Oktoba 12 mwaka huu) kusaka
pointi tatu. Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya
Polisi Dodoma na JKT Kanembwa ya Kigoma.
Pamba
na Mwadui zitacheza katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Polisi Tabora
itaikaribisha Toto Africans kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora
wakati uga wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma utatumika kwa mechi kati ya
Polisi Mara na Stand United ya Shinyanga.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)



0 comments:
Post a Comment