Waziri wa
Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohammed
amesema nchi yake itaendelea kushikamana na Tanzania katika kujenga Jumuiya
imara ya Afrika Mashariki.
Akizungumza
katika mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Waziri Amina
Mohammed ameisifu hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa bungeni Dodoma hivi
karibuni na kupongeza msimamo wa Tanzania wa kutojitoa katika Jumuiya hiyo.
Amesema Tanzania
na Kenya ni nchi waanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na amesisitiza
kwamba haiwezekani kujenga
Afrika Mashariki madhubuti kwa kuitenga Tanzania.
Waziri huyo
wa Mambo ya Nje wa Kenya aliwasili nchini jana jioni ambapo amekuwa na
mazungumzo ya faragha na mwenzake wa Tanzania, Bernard Membe katika masuala ya
Mustakabali wa Afrika Mashariki, Uhusiano wa Tanzania na Kenya na Kesi za ICC.
Hivi
karibuni, nchi tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda, Kenya na
Rwanda zimekuwa zikifanya mambo ambayo yameonekana kuzibagua Tanzania na
Burundi kiasi cha kuibua sintofahamu juu ya mustakabali ya Afrika mashariki
pamoja na hofu kuhusu utengamano wa jumuiya hiyo.
0 comments:
Post a Comment