Tatizo la
ugonjwa wa kisukari nchini (Diabetes) linaongezeka kwa kasi kubwa ambapo kwa
mujibu wa takwimu za mwaka 2000 asilimia sita ya watu mijini waligundulika kuwa
na ugonjwa huo hali ambayo inahitaji mikakati ya kukabiliana nao.
Kwa mujibu wa
matokeo ya utafiti ulifanyika nchini miaka ya themanini, wagonjwa wa kisukari
nchini kote vijijini na mijini walikuwa ni asilimia moja, ambapo utafiti wa
mwaka 2000 ulionyesha idadi hiyo kufikia asilimia 6 mijini na asilimia 1.6 vijijini.
Aidha takwimu
zinaonyesha kuwa hivi sasa, zaidi ya watu millioni mia tatu na hamsini duniani
kote wana ugonjwa wa kisukari na inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2030, watu million 530 duniani watakuwa na ugonjwa
huo.
Hayo
yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha magonjwa ya kisukari na moyo
cha St Laurent Dk Mary Mayige wakati wa kliniki ya wazi, na bure ya kupima
kisukari wakazi wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kituo
hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment