Nelson Mandela,
Msiba umetanda kote
ulimwenguni tangu zilipotangazwa habari za kifo cha Nelson Mandela.
Bendera
zimeshushwa nusu milingoti katika kila pembe ya dunia.
Na Siku hadi tatu za
maombolezi kutangazwa katika nchi nyingi duniani.
Viongozi wa kimataifa
wameelezea masikitiko yao na kusifu mchango wa Madiba kama mtu aliyekuwa
akipigania haki,uhuru na usawa ulimwenguni.
Rais Barack Obama wa Marekani
anasema kwa kufariki dunia Nelson Mandela,ulimwengu umempoteza mmojawapo wa
binaadam mwenye ushawishi mkubwa kabisa,mwenye moyo wa kijasiri kupita kiasi na
mwenye imani kupita kiasi.
Rais Obama ameungama maisha yake yasingekuwa kama
yalivyo ingekuwa dunia haijakuwa na mpinzani wa zamani wa Afrika kusini
aliyetumikia miaka 27 jela.
Rais Barak Obama amenukuu yale yaliyosemwa na Madiba
alipofikishwa mahakamani mwaka 1964 "Nimepigana dhidi ya utawala wa
kimabavu wa waupe na nimepigana dhidi ya utawala wa kimabavu wa watu
weusi.
Nnapigania maadili ya kuwepo jamii huru na ya kidemokrasia ambapo watu
wote wataishi pamoja kwa furaha na kuwa na fursa sawa.
Ni Maadili nnayotaraji
kuyaendeleza maishani mwangu na ikihitajika basi pi niko tayari kufa kwaajili
ya maadili hayo."
Matamshi kama
hayo yaetolewa pia na kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliyesema jina la
Nelson Mandela daima litafungamanishwa na mapambano ya wananchi wa Afrika
kusini dhidi ya unyonyaji na kupinduliwa utawala wa ubaguzi wa rangi na
mtengano Apartheid.
Miongo zaidi ya miwili jela haikumbadilisha Nelson wala
haikumtia chuki moyoni.Afrika kusini mpya imeibuka kutokana na wito wake wa
suluhu.
"Amesema kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Katibu mkuu wa
Umoja wa mataifa amemtaja Nelson Mandela kuwa ""Mtu asiyekuwa na
mfano katika kupigania haki.Hakuwa na kinyongo.Ameonyesha kinachowezekana
kutendeka katika dunia na katika kila mmoja wetu anasema katibu mkuu wa Umoja
wa mataifa Ban Ki Moon,aliyetoa nasaha watu wawe na imani na kushirikiana
kwaajili ya kupigania haki na utu.
Amerika kusini
rais wa Brazil Dilma Roussel amemtaja Nelson Mandela kuwa "mtu mashuhuri
mwenye ushawishi mkubwa kabisa wa karne ya 20.
Amesema Nelson Mandela ameongoza
utaratibu wa maendeleo katika historia ya binaadam kwa busara na
mapenzi-utaratibu uliopelekea kumalizika enzi za ubaguzi wa rangi na mtengano.
Malkia Eliabeth
wa pili wa Uingereza pia ameelezea masikito yake kutokana na kifo cha Nelson
mandela akisifu juhudi zake .Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza anasema
tunanukuu:"Juhudi zake ndizo zilizopelekea kuwepo Afrika kusini yenye
amani hii leo.
Na waziri mkuu wa Uingereza
David Cameroun anasema:"Nelson Mandela hakuwa shujaa wa wakati mmoja tu ni
shujaa wa enzi zote."
Waziri mkuu wa
India ,Manmohan Singh amemtaja Nelson Mandela kuwa kiongozi aliyefuata kweli nyayo
za Mahatma Gandhi.
Sifa na
maombolezi yametolewa pia na viongozi wa Ufaransa,Australia,Mashariki ya kati
na Latin Amerika kusifu mchango wa Nelson Mandela nchini mwake na ulimwenguni.
Mwandishi:Hamidou
Oummilkheir/Rduters/AFP
0 comments:
Post a Comment