Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi
Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.
Dkt. James
P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi
sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani.
Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-
ELIMU:-
· Masters in
Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani
(2008)
· PhD
(Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo
Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
· MSc
(Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
· BSc(Hons)
(Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994
UZOEFU WA KAZI:-
· Mwaka 2004 –
hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
· 2001 – 2004,
Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
· 2000 – 2001,
Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
· 1999 – 2000,
Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
· 1994 – 1999 -,
Exploration Geologist, Anglo America Corporation.
Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta
na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja
na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil),
Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.
Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa
sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao
walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.
Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake
na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO
ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe
kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni
mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
18
Desemba, 2014
0 comments:
Post a Comment