Licha ya wananchi kuwa wakipaza sauti zao
haswa katika suala zima la mamlaka husika kufanya ukaguzi wa mabasi ya
abiria,malori ya mizigo pindi yanapo fanya safari zake imeonekana bado kufuati
baadhi ya magari hayo kuharibika sehemu ambazo ni hatarishi na kutiliashaka kwa
wasafiri.
Hali hiyo inakuja baada ya watumiaji wa
barabara kuu ya Dar es salaam tunduma kujikuta katika wakati mgumu baada ya kukwama kwa
takriban siku nzima katika eneo la mlima kitonga baada ya gari moja kuharibika
katikati ya mlima huo na kufunga bara bara hiyo.
Baadhi ya abiria waliozungumza na TAMBARARE
HALISI wameiomba serikali kuweza kutanua njia ambazo ni ndogo haswa eneo hilo
la kitonga ambalo limekuwa sugu na ikiwa
eneo hilo si salama sana pindi gari linapo haribika ,
pamoja na kuweza kuweka
huduma maalumu ya kuweza kunasua magari kama hayo yakikwama ikiwemo gari la
kuvuta(Break Down) ambalo linaweza kusaidia na kutokuwepo na foleni kama
ilivyokuwa msongamano mkubwa baada ya gari hilo kukwama.
0 comments:
Post a Comment