Nchini Kenya waalim
wamechukua uamzi wa kurejea shuleni leo Jumatatu baada ya kuitikia mgomo
ulioitishwa na vyama vya waalim, mgomo ambao umedumu wiki mbili. Wazazi wa
wanafunzi na mashirika yanayotetea haki za watoto na wanafunzi yamepongeza
hatua hiyo ya waalim.
Mgomo
huo uliitishwa na chama cha Umoja wa Waalimu KNUT pamoja na KUPPET tangu
mwanzoni mwa mwaka wa shule, wiki mbii zilizopita, ambapo viongozi vyama hivyo
vya waalim waliwataka wanachama wao kutoripoti kazini kuanzia siku ya Jumatatu
ya tarahe 5 Januari mwaka 2015.
Chama
cha wazazi nchini Kenya kilikua kimewasilisha kesi mahakamani kutaka kuzuiwa
mgomo huo, uamuzi uliotangazwa na katibu mkuu wake, Musau Ndunda, ambaye
amesisitiza kutofumbia macho mgomo huu.
Awali
katibu mkuu wa KUPET, Akelo Missori, alitupilia mbali madai ya chama cha wazazi
na kuongeza kuwa hawatishwi na amri iliyotolewa na Mahakama kuwataka kusitisha
kwa muda mgomo walioanzisha.
Siku
moja tu baada ya mgomo huo kuanza serikali ilianzisha mazungumzo na vyama vya
waalim ili kujaribu kumaliza mgomo huo nchini Kenya, bila mafanikio. Chama cha
waalimu wa sekondari kimekua kikiidai serikali kiasi cha shilingi za kenya
bilioni 47, lakini srikali ya Kenya ilikua ilikataa kutoa pesa hizo.
Awali serikali
ilibaini kwamba ilikua ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 9.3 kama posho kwa
waalimu hao, kiasi ambacho kilipingwa na viongozi wa Kuppet hali iliyofanya
mazungumzo kati yao na serikali kukwama kama ilivyotokea siku ya Jumanne
Januari 6 mwaka 2015 kwa waalimu wa shule za msingi.
Waziri
wa kazi nchini Kenya, Kazungu Kambi alikua alisitiza kuwa serikali haina fedha
za ziada kutimiza madai ya walimu na kwamba iwapo watatekeleza madai hayo sekta
nyingine zitaathirika kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment