Wapiganaji wa Boko Haram waliendesha mashamulizi Jumapili Januari 18
kaskazini mwa Cameroon. Zaidi ya wapiganaji mia moja walishambulia vijiji
viwili viliyokaribu na mji wa Mokolo katika jimbo la kaskazini mwa Cameroon.
Wapiganaji hao walifaulu kuwateka nyara zaidi
ya watu themanini. Hata hivyo watu 24 miongoni mwa mateka hao waliachiliwa
huru, baada ya majeshi ya Cameroon kujibu mashambulizi ya wapiganaji hao.
Mashambulizi hayo ya Boko Haram yaligharimu
maisha ya watu watatu, huku uharibifu mkubwa ukishuhudiwa katika vijiji hivyo
viwili. Zaidi ya nyumba 80 zilichomwa moto.
Baada ya kutimuliwa na jeshi la Cameroon,
wapiganaji hao wa Boko Haram, walifaulu kupenya katika vijiji vya Mabassa na
Maky, na kupora vitu na mali viliyokua ndani ya nyumba. Takriban watu 80
walitekwa nyara, lakini 24 miongoni mwao waliachiliwa huru.
Mashambulizi hayo yanatokea wakati ambapo
Chad iliwatuma wanajeshi wake tangu Jumamosi Januari 17 mwaka 2015, ili
kushiriki katika mpango wa kikanda wa kuendesha vita dhidi ya Boko Haram. Kwa
mujibu wa msemaji wa serikali ya Cameroon, Issa Tchiroma Bakary, wapiganaji wa
Boko garam wamekua wakivuka mpaka kwa minajili ya kutafuta chakula.
"
Hali hiyo haitachukua muda mrefu, kwani nchi za ukanda huu zimeshikamana kwa
kwa kulidhibiti kundi hilo”, amesema Issa Tchiroma Bakary.
Lengo la kutumwa kwa majeshi ya Chad ni
kuurejesha mji wa Baga kwenye himaya ya serikali ya Cameroon. Mji wa Baga ni
mji muhimu wa jimbo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.
0 comments:
Post a Comment