Image
Image

Watoto 50 watekwa nyara na watu wenye silaha nchini Cameroon




Watu watatu wameuawa na watoto 50 kutekwa nyara nchini Cameroon na watu wasiojulikana wakati waliposhambulia jimbo la Far North la nchi hiyo.

Chanzo cha habari kutoka jeshi la serikali la Cameroon kimesema, washambuliaji pia wameharibu nyumba 80 na kupora ng'ombe 150.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na tukio hilo, ingawa kuna tetesi kuwa huenda shambulizi hilo lilifanywa na wapiganaji wa kundi lenye siasa kali "Boko Haram", kwa lengo la kulipa kisasi kufuatia serikali ya Chad kupeleka vikosi vyake nchini Cameroon kusaidia kupambana na kundi hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment