Watu
zaidi ya 40 waliokuwa safarini kutoka Tegeta kwenda ubungo wamenusurika kupoteza maisha baada ya
basi waliokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na lori lililoonekana kuwa ni la
jeshi na mmoja wa abiria kukatika baadhi ya viungo vyake vya mwili kufuatia
ajali hiyo.
Ajali
hiyo iliyotokea Tegeta ilizua taharuki
kwa wapita njia na abiria waliokuwamo ndani ya basi hilo aina ya Kosta huku
wengine wakipatwa na kiwewe cha kutaka kuruka kunusuru maisha yao huku
ikisababisha majeruhi wa ajali hiyo na umati wawatu ukiwa umezunguka kuona kile
kilichotokea.
Wakazi
wa tegeta na maeneo jirani waliguswa kwa hisia tofauti baada ya kufika hapo
katika eneo ilipotokea ajali ambapo walianza kutoa msaada kwa lengo la
kuwanusuru manusura kupoteza
maisha,baada ya Kosta hiyo kuonekana ikiwa imepondeka pondeka huku abiria
waliokuwa wamekaa mbele karibu na Dereva kuonekana kuumia zaidi ambapo kijana
mmoja aliyekuwa mbele alishindwa kutoka baada ya ajali nahivyo kufanyika
jitihada za kumnasua.
Msaada
wa kunasua majeruhi wa ajali hiyo waliokuwa wamebanwa ilifanywa na wasamaria
wema Mafundi Gereji wa Tegeta huku
wakitumia kifaa maalumu cha kukata mabati ya magari kukata bati la Kosta hiyo
na hivyo kuweza kunusuru maisha ya abiria hao ingawa wengine kuionekana kuwa
tayari baadhi ya viungo vya miili yao kuumia kutokana na kubanwa kwa muda na
bati la Kosta hiyo kwa muda mrefu.
Tambarare
Halisi Iliweza kumtafuta kamanda wa polisi wilaya ya kinondoni Kamilius Wambura kuzungumzia ajali hiyo ambapo
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema taarifa zaidi juu ya ajali
hiyo ataitoa baada kufanyika kwa uchunguzi wa kuweza kubaini kiini cha ajali.
Hata
hivyo Baadhi ya Mashuda wa ajali hiyo wamesema kuwa kutokea kwa ajali hiyo
kumetokana na Dreva walori hilo kushindwa kuweka tahadhari katika eneo hilo
hadi kutokea ajali ambayo ingesababisha vifo vya zaidi ya mamia ya watu.
Aidha
Madereva wa njia hiyo ya Tegeta wamepaza sauti zao kupitia ajali hiyo nakusema
kuwa ipo haja ya serikali kuangalia namna ya kuweza kuweka njia ya Mzunguko
maarufu kama(Round About)Lengo kubwa likiwa kunusuru ajali na pia kwa mabereva
wanao kuwa wakigeuzia katika eneo hilo la Tegeta kwa Dharura,na hivyo kusema
kufanya hivyo kuta saidia katika suala hilo la kutokea kwa ajali na hivyo
kuwasisitiza askari wa usalama bara barani kuangalia endapo kutakuwa na magari
Aina ya lori kama hilo waweze kuchukua tahadhari mapema kabla Haijatokea ajali
inayogharimu maisha ya abiria wasio na Hatia.
0 comments:
Post a Comment