Wafugaji 266 wa kijiji cha Mabwegere wilayani Kilosa mkoani
Morogoro hawana makazi baada ya nyumba zao kuchomwa moto na wakulima.
Nyumba hizo zimechomwa moto baada ya
kuzuka kwa mgogoro wa ardhi ambapo nyumba 38 zimeteketea kabisa na mazao
ya chakula kuharibiwa huku baadhi ya wanawake na watoto
wakilazimika kukimbilia kanisani kuomba hifadhi.
Wakizungumza kwa uchungu wanawake hao na
watoto wamelalamikia baadhi yao kubakwa na kufanyiwa ukatili na wengine
hadi sasa hawajulikani walipo ambapo wameeleza kupata hasara kubwa
ya kuchomewa nyumba zao huku wakiiomba serikali kutizama upya
mgogoro huo wa wakulima na wafugaji ili haki itendeke kwani
mgogoro huo unawaumiza wanawake na watoto.
Tambarare halisi ilitembelea maeneo ya
nyumba zilizochomwa moto na kukuta baadhi ya nyumba zikiendelea kuungua
huku vyakula navyo vikiteketea kwa moto ambapo mwenyekiti wa
kijiji na baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo wamesema chanzo cha
mgogoro ni wakulima kuingia kwa nguvu katika mashamba ya
kijiji cha wafugaji.
Baadhi ya vijana wa kimasai yaani morani
wameonekana msituni wakiwa na silaha za jadi ambapo wamesema wanawasaka
wakulima waliohusika na tukio hilo na kuendelea kulinda mipaka ya kijiji
kuzuia wakulimawasiingie kwa nguvu.
Jeshi la polsi mkoa wa morogoro limethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na askari wameonekana wakiwa na silaha
wakiimarisha ulinzi katika kijiji cha Mabwegere
0 comments:
Post a Comment