Hata hivyo kutangazwa kwa matokeo hayo
kunakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na baadhi ya vituo vya kupigia
kura kushindwa kupiga kura jana, na hivyo kufanyika leo.
Vituo hamsini na moja vitapiga kura hii leo
na sababu kubwa ni mvua kubwa iliyo nyesha nchi yote ya Zambia ,hali mbaya ya
hewa na kucheleweshwa kwa karatasi za kupigia kura ni sababu zilizotajwa
kusababisha wananchi wa Zambia kutopiga kura na leo wapewe haki hiyo.
Hali mbaya ya hewa pia huenda ikasababisha
hata matokeo ya uchaguzi kutolewa kama ilivyosemwa awali,naye Rafael
Phiri,msemaji wa tume ya uchaguzi ya Zambia amethibitisha kuwa endapo
yatachelewa sana haitazidi tarehe ishirini na nne mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment