Kansela Angela Merkel
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anatazamiwa
kushiriki maandamano ya jamii ya Waislamu leo hii kukuza suala la uvumilivu
katika jamii na kulaani mashambulizi yaliofanywa na Waislamu wa itikadi kali
mjini Paris.
Rais
Joachim Gauck atahutubia katika maandamano hayo yatakayoanza saa moja usiku
katika eneo mashuhuri la Lango la Bradenburg mjini Berlin maandamano
yaliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani chini ya beramu
"Kuwepo mashirikiano.Ugaidi sio jina letu".
Merkel
ambaye atakuwepo takriban na baraza lake lote la mwaziri katika maandamano hayo
amelishutumu kundi la siasa kali za mrengo wa kulia linalojiita Wazalendo wa
Ulaya Dhidi ya Kusilimishwa kwa Ulaya au PEGIDA kwa kifupi na kusisitiza hapo
jana kwamba Uislamu ni sehemu ya Ujerumani.
PEGIDA
hapo jana iliwavutia waandamanaji 25,000 katika maadanano yake ya 12 ya kila
wiki mjini Dresden mji ulioko mashariki mwa Ujerumani ambayo zamani ilikuwa
chini ya utawala wa Kikomunisti. Wafuasi wake waliokuwa wakipeperusha bendera
walibaki kimya kwa dakika moja kutowa heshima zao kwa wahanga wa mashambulizi
ya gazeti la Charlie Hebdo mjini Paris wiki iliopita.
Maandamano
Maandamano
yao hayo yalikabiliwa na maandamano mengine yanayowapinga yaliohudhuriwa na
watu 100,000 nchíni kote ambao wanaishutumu PEGIDA kwa kutumia vibaya kwa faida
yao mashambulizi hayo yaliofanywa na Waislamu wa itikadi kali nchini Ufaransa
ambapo wameelezea kuunga mkono kwao kuwepo kwa jamii ya tamaduni tafauti nchini
Ujerumani.
Merkel
na msimamo
Merkel
hapo jana amewashukuru viongozi wa jamii ya Waislamu milioni nne wanaoishi
Ujerumani kwa kulaani kwa haraka bila ya ajizi mauaji yaliofanyika kwa kutumia
jina la dini yao mjini Paris wiki iliopita.
Amesema
katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari uliohudhuriwa pia na Waziri
Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu kwamba Ujerumani inataka Waislamu waishi kwa
pamoja kwa amani na wafuasi wa dini nyengine na kwamba maandamano ya leo usiku
yatatowa ujumbe mzito.
Merkel
na Davotoglu wiki iliopita waliungana na Rais Farncois Hollande wa Ufaransa na
viongozi wengine duniani katika maandamano makubwa kabisa ya mshikamano mjini
Paris kufuatia mauaji ya watu 17 katika ofisi ya gazeti la dhihaka lilitolewalo
kila wiki la Charlie Hebdo na katika tukio la kushikiliwa watu mateka katika
duka moja la Kiyahudi.
Katika
taarifa yao Baraza la Waislamu na jamii ya Waturuki nchini Ujerumani wakati
wakilani mashambulizi hayo ya Paris wamesema kuzuka kwa wimbi jipya la ubaguzi
na chuki dhidi ya Uislamu katika mitaa ya Ujerumani kunazidi kuwapalilia
wachochezi na magaidi .
Maoni
yaliyotolewa kwenye mtandao wa gazeti la Spiegel nchini Ujerumani yamempongeza
Merkel ambaye anajulikana sana kwa kutoyalazia damu masuala nyeti kwa kutowa
kauli ya wazi kulaani chuki dhidi ya Uislamu hata kama anahatarisha kukipotezea
wapiga kura chama chake cha kihafidhina.
0 comments:
Post a Comment