TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard
K. Membe (Mb) ameondoka nchini tarehe 13 Januari 2015 kwenda Urusi
kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya
Nje wa Urusi, Mhe. Sergey Lavrov. Ziara hiyo inalenga kuimarisha na
kupanua ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.
Mhe. Membe anatarajiwa
kutumiafursa hiyo kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na Urusi, hususan
katika maeneo ya biashara, uwekezaji na ubadilishanaji wa teknolojia.
Tanzania inaweza kufaidika na utaalamu wa Urusi katika sekta za uzalishaji wa
nishati, uvuvi, afya, kilimo na huduma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
Tarehe 14 Januari, 2015.
Tarehe 14 Januari, 2015.
0 comments:
Post a Comment