Tanzania
imesema kuwa ni jambo la kusadikika na kufikirika tu kwa baadhi ya watu kudai
kuwa haiko tayari kukabiliana na vikundi vya uasi na ugaidi (negative
forces) vilivyobakia vikivuruga amani na kusababisha ukosefu
wa utulivu ndani ya nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Badala
yake, Tanzania inaendelea kuwa tayari kukabiliana na vikundi hivyo, kwa mujibu
wa mamlaka ambayo majeshi yake pamoja na yale ya Afrika Kusini na Malawi,
yamepewa na Umoja wa Mataifa (UN) ya kuvishambulia, kuvimaliza nguvu na
kuvinyang’anya silaha (neutralize and disarm all
negative forces) vikundi hivyo vyote.
Nchi
hizo tatu zinaunda Brigedi ya Kimataifa ya Force
Intervention Brigade (FIB), ambayo ni
sehemu ya Majeshi ya UN katika DRC ya United
Nations Stabilisation Mission in Congo (MONUSCO), yaliyoko
chini ya Luteni Jenerali Alberto Santacruz wa Brazil. Chini ya mamlaka ambayo
Brigedi hiyo imepewa na UN, majeshi ya nchi hizo tatu, yana uhalali wa
kuvishambulia vikundi vya kiasi katika DRC.
Msimamo
huo wa Tanzania umerudiwa tena na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Januari 13, 2015, alipokutana na
kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Novisise Mapisa-Nqakula, Mjumbe Maalum wa Rais
wa Afrika Kusini na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo. Waziri Nqakula amefuatana na
Waziri wa Usalama wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Mahlobo.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, wakati akiwatakia mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika
Tanzania Heri ya Mwaka Mpya wakati wa Halfa ya Mwaka ya Sherry Party
iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete aliyaeleza maoni na shutuma
dhidi ya Tanzania kuwa ni mambo ya “kudharauliwa”.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Zanzibar, Rais Kikwete amemwambia Bibi
Nqakula kuwa msimamo wa Tanzania umekuwa ule ule wa siku zote bila mabadiliko
yoyote – yaani kuhakikisha kuwa majeshi na vikundi vyote vya uasi ndani ya DRC
vinamalizwa. Rais Kikwete amekuwa Zanzibar tokea jana, Jumatatu, Januari 12,
2015 wakati alipohudhuria sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Bofya Kujua zaidihttp://www.ikulu.go.tz/index.php/media/press_details/1273


0 comments:
Post a Comment