Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bi Nkosazana Dlamini Zuma amelaani vikali mashambulizi yanayoendelea kufanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram katika maeneo mbalimbali nchini Nigeria na sehemu nyingine za Afrika.
Kwenye taarifa yake, Bi Zuma ameeleza
kushtushwa kwake na mauaji ya hivi karibuni katika soko la Potiskum kwenye mji
wa Baga jimboni Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Shambulizi hilo linadaiwa kufanywa na
washambulizi wawili wa kike wa kujitoa mhanga, huku mmoja akisemekana kuwa na
umri wa miaka 10.
Bi
Zuma ametoa salamu za rambi rambi kwa familia za wahanga na kusisitiza kuwa,
Umoja huo unasimama na watu pamoja na serikali ya Nigeria katika wakati huu
mgumu.



0 comments:
Post a Comment