Viongozi
hao wanatarajia kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa nchi mbili hizi
ikiwemo suala la reli ya Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA), inayounganisha Tanzania na Zambia.
Hivi
karibuni Reli ya TAZARA imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo
zinahitajika kujadiliwa kwa kina na viongozi wakuu ili kuimarisha zaidi reli
hiyo ambayo ni kiungo kikubwa baina ya nchi hizi katika masuala ya uchumi na alama ya ushirikiano.
TAZARA
ilizinduliwa rasmi Oktoba 1975 kwa ufadhili wa China. Reli hiyo ina upana wa
milimita 1,067 na urefu wa Kilometa 1, 860 kuanzia Dar es Salaam, Tanzania na
kuishia katika mji wa New Kapiri Mposhi nchini Zambia.
Reli
hiyo ina uwezo wa kusafirisha mizigo ya tani milioni 5 na watu milioni 3 kwa
mwaka.
Rais
Kikwete na ujumbe wake wanatarajiwa kurejea nchini kesho tarehe 26 Februari,
2015
……………MWISHO……………
Imetolewa na:
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
25
Februari, 2015
0 comments:
Post a Comment