Kutoka Dodoma - Bungeni
Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema serikali inaangalia
utaratibu utakaowawezesha watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza kupiga kura
katika uchaguzi Mkuu wa wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka
huu.
Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi huo bungeni mjini DODOMA wakati akijibu maswali ya
papo kwa papo kutoka kwa baadhi ya wabunge waliotaka kujua maandalizi
yaliyofanywa kuwawezesha watanzania hao watekeleze demokrasia yao kuchagua
viongozi.
Waziri Mkuu PINDA amesema suala la maandalizi ya uchaguzi yakiwemo ya
kuwashirikisha watanzania waliopo nje linashughulikiwa na Tume ya Taifa ya Tanzania
Bara -NEC na Tume ya Uchaguzi ZANZIBAR - ZEC.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment