Toleo la pili baada ya shambulio katika makao makuu ya gazeti la Charlie Hebdo litatolewa tarehe 25 mwezi huu.Mhariri mpya wa gazeti la Charlie Hebdo amefahamisha kuwa katika toleo lake lijalo litakalotolewa Februari 25 halitokuwa na kibonzo cha Mtume Muhammad.Gazeti la Charlie Hebdo litachapisha toleo lake la pili baada ya shambuliyo katika makao makuu yake jijini Paris ambalo watu 12 waliuawa mnamo Januari 7.Gazeti hilo lilichapisha kibwengo cha Mtume Muhammad katika toleo lake la kwanza baada ya shambulio hilo.Mhariri mpya wa gazeti hilo alifahamisha kuwa toleo lijalo halitokuwa na kibwengo cha mtume na kuwataka wateja wake wawe na uvumilivu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment