Mlemavu wa ngozi akiwa anaonekana na majeraha mbali mbali
katika mwili na mikono yake baada ya kuwa amejeruhiwa na watu ambao wana wateka
na kuwaua watu wenye ulemavu huo(Picha na Maktaba Yetu).>>> http://www.itv.co.tz/news
Serikali ya mkoa wa Mwanza
imetangaza vita dhidi ya wahalifu wanaojihusisha na maua ji ya walemavu wa ngozi
na kusababisha hofu kubwa kwa watu wenye UALBINISM ambao wameshindwa
kufanya kazi za maendeleo wakihofia usalama wa maisha yao baada ya kumeibuka
kundi la wahalifu la kupora watoto wadogo wenye ulemavu wa ngozi na kuwachofoa
viungo vya miiliyao kutokana na imani potofu za kishirikina.
Tamko hilo limetolewa na
kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Mchungaji Baraka Konisaga wakati akizungumza na ITV
katika hospitali ya rufaa bugando baada ya kumuona majeru hi aliyevamiwa na
wahalifu nyumbani kwake katika kijiji cha ilelema kata ya ipalamasa wilayani
chato mkoani geita BI.ESTER JONAS ambaye kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya
rufaa bugando jijini mwanza.
Kwa upandewake mkurugenzi
wa hospitali ya rufaa Bugando PROF KIEN MTETA amesema uongozi wa hispitali
hautamtoza gharama za matibabu mgonjwa BI.ESTER JONAS na kwamba kumeanzishwa
kampeni maaluma ya kuhamasisha jamii itambue umhimu wa kuwalinda walemavu wa
ngozi ambapo muuguzi kitengo cha ent agineta mtatebwa amesema hali ya mgonjwa
inaendelea vizuri anaweza kukaa,kula chakula laini na kuzungumza.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment