Image
Image

Baba wa marehemu AK47 ataka polisi kuharakisha uchunguzi wa Kifo cha mwanae


Baba wa msanii Emmanuel Mayanja Hummertone maarufu kama AK47, Mzee Gerald Mayanja amesema anataka majibu kuhusu nini kimemuua mtoto wake huyo na kuwaomba polisi kuharakisha uchunguzi wa kifo chake.

Mzee Mayanja ametoa kauli hiyo huko maziko ya mwanae AK47 yakipangwa kufanyika kesho huko Mityana, ambapo mwili wake uliwekwa jana jioni katika eneo la National Theatre kwa ajili ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho.

Watu wengi walijitokeza jana National Theatre kuungana na familia ya Mzee Mayanja katika kuomboleza kifo cha ghafla cha AK47, ambapo huzuni zilitawala katika eneo lote la viwanja vya National Theatre.

Emmanuel Mayanja ambaye ni mdogo wa msanii nyota wa Uganda Jose Chameleone alitangazwa kufariki dunia katika hospitali ya Nsambya, baada ya kudaiwa kuanguka akiwa chooni kwenye klabu ya DEJAVU iliyopo Kansanga.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment