Image
Image

Rais Jacob Zuma anusurika kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye bungeni


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini jana amenusurika katika zoezi la bunge kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Hoja hiyo ililetwa bungeni na mbunge wa chama cha upinzani cha DA, Mmusi Maimane, iligonga mwamba baada ya wabunge wengi wa chama tawala cha ANC kuipinga.

Jumla ya kura 221 zilipinga hoja hiyo, huku kura 113 zikiunga mkono, katika zoezi la upigaji kura lililolazimika kuchelewa kwa muda baada ya kubaini mfumo wa kupigia kura wa kielektroniki kushindwa kufanya kazi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment