Ni swali linaloulizwa na Umoja wa Mataifa ukielekea kwenye maadhimisho ya siku ya furaha duniani, tarehe 20 Machi.
Kwa maana hiyo Umoja wa Mataifa umezindua kampeni kwenye mitandao ya kijamii inayoitwa ''#HappySoundsLike''
yaani “Sauti ya Furaha” ukiiomba jamii ya kimataifa kuchagua wimbo bora unaomfanya mtu kufurahi zaidi.
Katika uzinduzi wa kampeni hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
amewaomba watu wote kuwa na furaha, katika lugha rasmi zote sita za
Umoja wa Mataifa.
“Kwenye siku hii, tunatumia lugha ya kimataifa
ya muziki kuonyesha mshikamano na mabilioni ya watu duniani
wanaoathirika na umaskini,
ukiukwaji wa haki za binadamu, mizozo ya kibinadamu na matokeo ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi”
Aidha
amesema kwa upande wake wimbo anoupenda zaidi ni “Signed Sealed
Delivered” wa Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa, Stevie Wonder.
Tungo zitakazochaguliwa na watu zitachezwa katika orodha maalum itakayoandaliwa na kampuni ya muziki ya MixRadio.
Miongoni mwa wasaani watakaoshiriki kwenye maadhimisho hayo mwishoni mwa wiki hii mabalozi wa umoja wa mataifa
Charlize
Theron, Lang Lang, Michael Douglas, Midori, Jean-Michel Jarre na
Angelique Kidjo pamoja na wasaani maarufu kama David Guetta, Cody
Simpson na Pharrell Williams.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment