Chama cha Likud cha Waziri Mkuu wa Israeli Bwana BENJAMIN NETANYAHU kimepata ushindi wa kushangaza katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo na hivyo kumuwezesha kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa nne.
Utabiri wa awali ulionyesha vuta nikuvute kwa ushindani wa karibu lakini baada ya karibu kura zote kuhesabiwa matokeo yamekipa chama cha Likud ushindi wa wazi dhidi ya chama kikubwa cha upinzani cha mrengo wa kushoto cha Zionist Union.
Matokeo hayo ambayo mpaka sasa chama cha Likud kina viti 30 katika bunge la viti 120 na Chama cha Zionist Union kina viti 24 na hivyo kumpa Bwana NETANYAHU nafasi kubwa ya kuunda serikali ya mseto ya mrengo wa kulia na kuwa Waziri Muu wa kuongoza nchi hiyo kwa muda mrefu.
Kiongozi wa Chama cha Zionist Union Bwana YITZAK HERZOG amempigia simu Bwana NETANYAHU kumpongeza na kumtakia kila la kheri.
Home
Kimataifa
Waziri Mkuu wa Israeli Bwana BENJAMIN NETANYAHU kuongoza sasa nchi hiyo kwa muhula wa nne baada ya kushinda
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment