Naibu Waziri wa uchukuzi DKT.CHARLES TIZEBA amezihakikishia kaya zaidi
ya 500 zenye makazi katika eneo la Mlima KISEKE jijini MWANZA kuwa
makazi hayo ni salama kwa afya zao kinyume na hofu iliyokuwa imetanda
siku za nyuma kutokana na ujenzi wa rada katika mlima huo.
DKT.TIZEBA ametoa ufafanuzi huo mjini MWANZA kufuatia kaya hizo kujawa na wasiwasi zikitakiwa kuhama ili kunusuru afya zao.
Eneo la Mlima kiseke uliopo wilaya ya ilemela mkoani mwanza ndiko
ambako rada ya kisasa ya utabiri wa hali ya hewa imejengwa ili
kuimarisha shughuli za utabiri wa hali hewa katika mikoa ya kanda ya
ziwa.
Kujengwa kwa rada hiyo kumesababisha zaidi ya kaya mia tano
zinazozunguka mlima huo kuendelea kuishi kwa hofu ya kukumbwa na athari
zitokanazo na mionzi ya rada ikiwemo ugonjwa wa saratani.
Hofu ya wakazi hao imefuatia matamko kadhaa yaliyotolewa mwaka mmoja
uliopita na viongozi wa serikali wakiwemo wa mamlaka ya hali ya hewa ya
kuzitaka kaya hizo kuhama ili kunusuru afya zao.
Mwaka mmoja baada ya kauli hizo,naibu waziri wa uchukuzi DKT.CHARLES
TIZEBA amekutana na waandishi wa habari jijini mwanza na kuwaondoa hofu
wakazi hao kwa kueleza kwamba mionzi ya rada hiyo haina madhara kwa
afya za wakazi wa eneo hilo swala lililo ungwa mkono na mhandisi LENY
MGANGA ambaye ni meneja mradi wa rada hiyo.
Rada hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi billion 3 na
milioni mia sita pia inakabiliwa na tishio la uendelevu kutokana na
shughuli za kibinadamu zinazoendelea kwenye mlima huo
Home
News
Naibu waziti TIZEBA amezihakikishia kaya zaidi ya 500 zenye makazi katika eneo la Mlima KISEKE jijini MWANZA kuwa makazi hayo ni salama kwa afya zao
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment