Kanisa hilo ambalo linashirikisha idadi kubwa ya wanachama wake duniani lilitoa tangazo hilo baada ya idadi kubwa ya magavana wa majimbo yake 171 kuidhinisha mabadiliko hayo.
Sheria yake mpya sasa itasoma kwamba ndoa ni makubaliano ya kipekee kati ya watu wawili ikilinganishwa na makubaliano kati ya mume na mke.
Sheria hiyo ilioidhinishwa na baraza kuu la kanisa hilo mwaka uliopita ilikubaliwa na zaidi ya nusu ya majimbo ya kanisa hilo.
Mkutano wa makundi katika jimbo la New Jersy ulikuwa wa 86 kuidhinisha sheria hiyo.
Uamuzi huo unatarajiwa kuzua mgawanyiko mkubwa kati ya wanachama wa kanisa hilo ambao wanapinga sheria hiyo.
Mwaka uliopita baraza kuu la kanisa hilo lilitoa idhini kwa wachungaji wake kuwafungisha ndoa wapenzi wa jinsia moja katika majimbo ambayo ndoa hizo zinaruhusiwa.
0 comments:
Post a Comment