Rais
Mstaafu wa awamu ya Tatu nchini Tanzania Mh. BENJAMIN MKAPA amezindua
rasmi Kavazi la Mwalimu Nyerere,kituo huru kilichoanzishwa ndani ya Tume
ya Sayansi na Teknolojia Tanzania chenye majukumu makubwa matatu.
Jukumu
la kwanza ni kuhifadhi nyaraka zilizokusanywa na waandishi wa
Bayografia ya Mwalimu NYERERE ili zitumiwe na watafiti na pili ni kutoa
nafasi ya mijadala ya kizuoni na mikakati juu ya masuala muhimu ya
jamii.
Halikadhalika kituo hicho Kavazi la Mwalimu kinatakiwa kuandaa
na kuendesha mafunzo ya nadharia na mbinu za utafiti wa masuala ya
maendeleo.
Awali Mkurugenzi wa Kavazi la Mwalimu NYERERE Profesa ISSA
SHIRVJI alielezea zaidi kuhusu kituo hicho na kutaka viongozi hapa
nchini kujenga utamaduni wa kuhifadhi nayaraka zao.
Profesa ISSA
SHIRVJI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment