Image
Image

Licha ya kupataushindi wa magoli 2-0 dhidi ya monaco,hatimaye arsenal imekwama kuingia hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya


Pamoja na kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji wao Monaco katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora, matokeo hayo hayakuweza kukisaidia kikosi cha Arsenal kusonga mbele hatua ya robo fainali ya michuano hiyo yenye fedha nyingi barani Ulaya.
Arsenal imejikuta ikikwama kuingia robo fainali baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja wao wa nyumbani " Emirate " kukubali kufungwa na Monaco mabao 3-1.
Kwa matokeo ya mchezo huo uliochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Stade Louis jijini Paris, Monaco wamesonga mbele hatua ya robo fainali. 

Mabao ya Arsenal yaliwekwa kimiani na Olivier Giroud katika dakika ya36,na bao la pili likifungwa na Aaron Ramsey katika dakika ya 79.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akiwa kainama huku kashika kichwa chake wakati muda wa mchezoukiwa ukingoni. Benchi lote ni huzuni

Tizama muonekano wa uwanja wa Stade Louis unavyoonekana kabla ya mchezo kati ya Monaco na Arsenal kuanza.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment