Image
Image

Jinamizi la ajali latafuna watu wanane katika ajali ya barabarani huko Mikumi Barabara ya Iringa Morogoro.


Ikiwa zimepita takribani wiki mbili tangu ilipotokea ajali mbaya na yakutisha iliyoweza kugharimu maisha ya watu takrinbani 50 Wilayani Mufindi mkoani Mkoani IRINGA na kupelekea serikali kuundwa kamati mbili uangalizi wa mizigo ya abiria waliohusika kwenye ajali ya basi na lori hilo,Hatimaye ajali nyingine imetokea ambapo Watu wa nane wamefariki Dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali ya Basi la Luinzo lililokuwa likitokea njombe kwenda DSM kugongana na gari la Msanga EXPRESS lililokuwa likitokea morogoro kwenda Mahenge wakati likijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake katika Eneo la hifadhi ya Mikumi Barabara ya Iringa Morogoro.

Akizungumza na TAMBARARE HALISI Mwandishi wetu aliyekuwapo eneo ilipotokea ajali hiyo amesema kuwa chanzo kikubwa ni mwendo kasi wa gari hilo la Msanga Express ambalo lililikuwa linajaribu kupita lori hilo na hivyo kujikuta likisababisha ajali tatu kwa wakati mmoja.

Amesema kuwa kufuatia vifo vya watu hao nane waliopoteza maisha katika ajali hiyo nikwamba awali watu saba ndio waliothibitika kufariki dunia papo hapo na mmoja alikuwa hali yake ni mbaya na hivyo wakati anakimbizwa hospitali ya Misheni Senti Kizito iliyopo katika mji mdogo wa mikumi akafariki akiwa njiani.

Watu waliofariki na kujeruhiwa ni walikokuwamo katika gari Msanga Express ambalo lilikuwa mwendo kasi Hivyo Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Mikumi huku wakiwa na majeraha mbali mbali katika viunga vya miili yao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment