Mvua zilizonyesha Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo
zimesababisha adha kwa wakazi mbali mbali ya jiji na hivyo kufanya hali
ya usafiri kuwa mgumu na watu kuchelewa katika kulijenga taifa kwa wakati.
Pande za jiji kila mmoja amekuwa shuhuda wakusimulia hili
ingawa hofu ya mvua hii inaonesha kuwaweka shakani wakazi wa mabondeni ambao
serikali imekuwa ikiwasisitiza kuhama maeneo hayo kwakuwa sio rafiki mzuri wa
maisha ya mwanadamu.
Baadhi ya nyumba maeneo ya msasani imeelezwa kuwa hali
haikuwa shwari kwa mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo ambayo maji yameweza
kuingia majumbani mwa wakazi wa maeneo hayo nasehemu nyingine nahivyo kuharinu
baadhi ya vitu,hali ambayo si nzuri sana na inatia hofu endapo mvua hiyo
itaendelea.
Na Chini hapo ni Baadhi ya Ghari zikiwa kwenye foleni leo asubuhi huku mvua ikinyesha Eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakazi wa jiji wamezungumza na TAMBARARE HALISI
Nakusema kuwa mvua hii inaonesha inanyesha kwa kusuasua kwani wakati inaonyesha
kunyesha na hainyeshi hivyo ikinyesha bila kuwa na taarifa na kiwango cha mvua
kinaweza kuleta madhara ya mafuriko kama yaliyokuwa yametokea na kuhatarisha
maisha ya wakazi waishio mabondeni.
Hata hivyo wameiomba mamlaka ya hali ya hewa nchini kuweza
kuzungumza nmamna mvua hizi zitakavyokuwa zikinyesha na hata ukomo wake ili
kuweza kuchukua tahadhari mapema kabla hayajatokea makubwa.
Hata hivyo wameiomba mamlaka ya hali ya hewa nchini kuweza
kuzungumza nmamna mvua hizi zitakavyokuwa zikinyesha na hata ukomo wake ili
kuweza kuchukua tahadhari mapema kabla hayajatokea makubwa.
Hivi ndivyo hali ionekanavyo kwa mvua iliyonyesha usiku wa muamkia leo hii katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam,Hapa Ni Bamaga Mwenge.Na Chini hapo ni Baadhi ya Ghari zikiwa kwenye foleni leo asubuhi huku mvua ikinyesha Eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment