Spika wa Bunge Mhe.Anna
Makinda amesema bunge linalaani vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye
ulemavu wa ngozi yaani Maalbino vinavyoendelea hapa nchini.
Hayo yamejiri bungeni wakati spika Makinda akitoa kauli ya bunge kuhusiana na
maelezo binafsi ya mbunge wa viti maalum ambapo pamoja na mambo mengine
ameziomba mahakama kuharakisha utoaji wa hukumu wa kesi zinazohusiana na
kuwajeruhi ama kuwaua maalbino.
Amesema ni jambo ambalo haliingii akilini kwa watu kudhania kuwa viungo vya
wenzao vinaweza kuwapatia utajiri hivyo ni bora jamii ikapambana kutokomeza
vitendo hivyo.
Awali Mhe.Shaymar amesema hali ya maisha ya maalbino kwa sasa nchini
imekuwa tete kwani wanaishi maisha ya mashaka huku wakiwa hawajui hatma ya
maisha yao.
0 comments:
Post a Comment