Rais BARACK OBAMA ametoa wito kwa
watu wa Nigeria kuacha vurugu
katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii.
Rais OBAMA amesema Nigeria
inapaswa kufanya u chaguzi ulio huru na wa haki na bila ghasia za aina yoyote ile kwani watu wa
napaswa kupiga kura zao bila ya vitisho
ama wasi wasi.
Kwa sababu hiyo ametoa wito kwa
viongozi wote na wagombea kuzungumza na
wapiga kura wao kwamba vurugu hazina nafasi katika uchaguzi wa
kidemokrasia.
Wasi wasi wa hali ya usalama
imezidi k uongezeka Nigeria kadri siku ya
uchaguzi inavyokaribia huku kukiwa na mvut ano mkali kati ya Rais
GOODLUCK JONATHAN wa chama tawala cha
PDP na mgomb ea wa upinzani wa chama cha APC
kiongozi wa zamani wa kijeshi Jenerali MUHAMMADU BUHARI.
0 comments:
Post a Comment