Maonyesho hayo yatakayofanyika jijini hapa Juni
mwaka huu, yatatanguliwa na semina kwa wafanyabishara mbalimbali ili
kuwajengea uwezo wa kubuni mradi mikubwa itakayoweza kupata wawekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIPEC Rodgers Mbaga
aliwaambia waandishi habari leo kuwa, wamefikia hatua hiyo baada ya
kuona kwamba wafanyabishara wengi wanafikiria kuwa na miradi midogo
wakati zipo fursa nyingi zaidi katika miradi mikubwa.
Alisema, maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwa
mara ya kwanza jijini hapa yanalenga wafanyabishara wenye miradi
isiyopungua dola za Kimarekani 250,000 sawa na Sh 500 milioni za
Kitanzania.
“Tunataka wafanyabiashara wetu na wamiliki wa
miradi mikubwa, kufikiria kuwa na ndoto kubwa ili waweze kupata
mafanikio makubwa lakini pia kuwavutia wawekezaji wanaopenda kuwekeza
kwenye miradi mikubwa,”alisema Mbaga na kuongeza kuwa hakuta kuwa na
kuuza bidhaa.
Alisema, kabla ya maonyesho hayo wafanyabishara
binafsi na wataasisi binafsi watapewa semina inayolenga kuwajengea uwezo
wa kutayarisha miradi ambayo itawavutia wawekezaji kutoka ndani na nje
ya nchi kwenye maonyesho hayo.
Ofisa Mwandamizi Ukuzaji Masoko wa kampuni hiyo,
Stephen Koberou, alisema maonyesho hayo yatasadia wafanyabishara kupata
wawekezaji kwenye miradi yao.
“Lakini ikifika kwenye utekelezaji fursa nyingine
kama ajira zitaongezeka, uzalishaji wa biadhaa zitakazokuwa zinauzwa
ndani na nje ya nchi utaongezeka,”alisema Koberou na kuongeza hayo yote
ni mchango katika kukuza uchumi wa nchi.
Naye, Mwakilishi kutoka Baraza la Taifa la
Biashara, Victoria Hingira alisema, watahakikisha kuwa wanashirikiana na
TIPEC ili miradi ya wafanyabiashara iweze wawekezaji.
0 comments:
Post a Comment