Ndege ya Shirika la Ndege la Ujerumani
la German-wingsaina aina ya Airbus A320 ikiwa na abiria 142 na wahudumu wa
ndege sita imeanguka nchini Ufaransa kati ya eneo la Barcelonnette na Digne.
Maafisa wa Mamlaka ya Usalama wa
Ndege nchini Ufaransa kwa kushirikiana na polisi imesema ndege hiyo ilikuwa
ikitokea Barcelona kwenda mji wa Dusseldorf nchini Ujerumani. Ndege hiyo
inamilikiwa na shirika mama la Lufthansa.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
amesema haijabainishwa jinsi ajali hiyo ilivyotokea lakini inapelekea kufikiria
kuwa hakuna mtu aliyenusurika kwenye ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment