Serikali imesema haina
mpango wa kufanya marekebisho ya katiba ili kufanya Marais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuweza kupatikana kwa zamu kati ya Tanzania bara na
Zanzibar.
Naibu waziri wa sheria na katiba Ummy Mwalimu amesema kufanya hivyo ni sawa na kuzorotesha Demokrasia hapa nchini hivyo kamwe hakutakuwa na mpango wa kurekebisha katiba katika kipengele hicho.
Naibu waziri wa sheria na katiba Ummy Mwalimu amesema kufanya hivyo ni sawa na kuzorotesha Demokrasia hapa nchini hivyo kamwe hakutakuwa na mpango wa kurekebisha katiba katika kipengele hicho.
Amesema kuruhusu kitendo hicho ni sawa na kuruhusu mgawanyiko katika nchi kwani
katiba ya hivi sasa imetoa uhuru wa upande wowote kugombea nafasi ya Urais kama
ana sifa kama zilivyoainishwa katika katiba ibara ya 39.
Katika hatua nyingine Spika wa Bunge mama Anna Makinda amekataa kuzungumzia
lolote kama kutakuwepo au la muswada wa vyombo vya habari katika mkutano wa 19
wa bunge la Jamhuri ya Muungano linaloendelea mkoani Dodoma.
Spika Makinda amefanya hivyo kufuatia ombi la muongozo kutoka kwa mbunge wa
Kisarawe Selemani Jafo aliyetaka kujua kama muswada huo utakuwepo au la katika
mkutano huu wa Bunge unaoendelea.
0 comments:
Post a Comment