Tawi kuu la chama cha wananchi CUF jimbo la
Dimani lilioko kisauni wilaya ya magharibi Zanzibar limeteketea kwa moto
na kuharibika kabisa huku chanzo chake ikiwa bado ni kitendawili kwa chama
hicho na Jeshi la Polisi Zanzibar.
Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi kamishna
msaidizi wa Polisi Mucadam Khamis Mucadam amemsmea Polisi imefika
katika eneo la tukio na kuanza upelelzi na moto huo ulianza wakati wa
usiku saa nane hadi sasa bado ni mapema kuzungumzia chanzo chake kwa vile bado
Polisi ianendelea na uchunguzi huku akisisitiza ustahimilivu wa kisiasa
Hata hivyo wakakti Polis ikendelea na uchungzi wake
chama cha waanchi CUF kupitia kwa mkurugenzi wake wa uenezi na uhusiano wa umma
Bw Salum Bimani amesema Tawi hilo limechomwa na watu waliokuwa na nia ya
maksudi kunfanya kitendohicho na hizo ni njama za kuitaka kukidhofisha chama
chao kulekea uchaguzi mkuu huku mwnyekiti wa CUF jimbo la Dimani
Bw. Ali Juma Ali amesema walinzi walioko karibu na tawi hilo wamedai
kuwaona watu wanne waliokuja na gari na inasemkana walivunja kufuli na
kuingia ndani na kuwasha moto na kuondoka.
Jengo la CUF likionekana likiwa limeungua leo katika jimbo la Dimani lilioko kisauni wilaya ya magharibi Zanzibar
tunatakiwa tustahamili sana ndugu zanguni kwani kuna watu wanataka kutufarakisha sisi nao si wengine ni viongoz wetu wenyewe kwa hiyo tuwe na akili zetu timamu
ReplyDelete