Watu sita wamefariki Dunia
na wengine tisa kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari manne likiwemo
basi la kampuni ya Super Shem lililokuwa likitokea jijini Dar-es-salaam
kuelekea mkoani Mwanza ambapo liligongana uso kwa uso na gari ya halmashauri ya
wilaya ya Nzega na kusababisha magari mengine mawili kugongana baada ya kukosa Muelekeo.
Ajali hiyo imetokea
katika barabara ya Mwanza – Dar-es-salaam eneo la kijiji cha Undomo kata ya
uchama wilayani nzega mkoani tabora.
Katika ajali hiyo inayodaiwa
kuwa chanzo chake ni mwendo kasi na baadhi ya madereva katika magari hayo
kutokuwa makini ambapo basi la Super Shem lenye nambari za usajiri T874 CWE
lililokuwa likitokea Dar-es-salaam liligongana uso kwa uso na gari aina ya LAND
CRUIZER lenye nambari za usajiri SM 4905 mali ya halmashauri ya wilaya ya nzega
ambapo watumishi watatu wa halmashauri hiyo walifariki dunia.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Bw.Patrick Mbozu anaeleza
namna walivyopokea tukio hilo la ajali lililosababisha majonzi na simanzi
Kaimu mganga mkuu
mfawidhi wa wilaya ya Nzega Dr.Erick Mbuguye anaeleza hali ya majeruhi
waliofikishwa hospitalini hapo na kulazwa.
Miili ya marehemu
iliyotambuliwa ni pamoja na aliyekuwa dereva wa gari la halmashauri
Charles Sanga,mhasibu wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Bw.Emmanuel
Kasenyi,Bwana afya wa wilaya Peter Steven,Robert Kisabho mtumishi wa
halmashauri,Yasinta Alex mkazi wa isunga na matukuta
malikita.
0 comments:
Post a Comment