Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitizama namna ambavyo maji yametuama kwenye nyumba Buguruni kwa mnyamani leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko.
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita katika mitaa mbalimbali ya Buguruni leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfereji ulioziba kutokana na uchafu na kusababisha mafuriko katika makazi ya watu eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni
Mnyamani leo.
Na.Msaka Noti.
Rais Jakaya Kikwete amefanya ziara
ya kushtukiza katika eneo la Buguruni Mnyamani ili kujionea madhara makubwa ya
mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam na kusababisha zaidi ya watu
1500 kukosa hifadhi baada ya nyumba zao kuingiwa na maji.
Baada ya Rais Kikwete
kuwasili katika eneo hilo la Buguruni
Mnyamani jijini Dar es salaam huku akizingirwa na umati mkubwa wa watu,baadhi
ya wakazi hao wamesikika wakipongeza ujio wa rais kufika katika eneo hilo ili
kujionea walivyokimbia makazi yao baada ya maji
kuingia katika nyumba zao na kuwalazimu kulala nje wakilinda mali zao.
Akizungumza na wakazi wa Buguruni
Mnyamani,Rais Kikwete amesema amelazimika kufika katika eneo hilo ili kuona
jitihada zinazofanyika za kuondoa maji hayo ili wananchi wawe salama huku akikisisitiza
kuwa baada ya maji hayo kuondolewa, ujenzi wa bomba mpya ambao ni mkubwa ufanyike
ili kusaidia kupitisha maji wakati wa mafuriko.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo
akiwemo mzee Saidi Mohamed Bakari amesema wanaishi maisha ya tabu na wana siku
saba hawajalala kutokana na maji hayo kuingia ndani ya nyumba zao.
0 comments:
Post a Comment