Jopo la Wataalamu washauri katika mkutano
uliokutanisha wadau mbalimbali ya sekta ya barabara nchini kujadili upembuzi
yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar - Chalinze.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)
Eng. Patrick Mfugale akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua
mkutano wa kujadili kuhusu upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa
barabara ya Dar - Chalinze uliofanyika jijini Dar es salaam.
Ramani ya barabara ya njia sita (tatu kila
upande) ya Dar es Salaam - Chalinze – Morogoro.
Tayari maandalizi ya ule mpango wa kujenga barabara ya
njia sita (tatu kila upande) Dar es Salaam – Chalinze-Morogoro (km 200) Express
Way umeiva ambapo awamu ya kwanza itahusisha barabara ya Dar es Salaam (Biti
Titi Jnct) – Chalinze (km 100) Express Way kwa utaratibu wa Public Private.
Barabara hiyo mbadala ambayo itakuwa ni ya kulipia itajengwa kwa njia sita (6 lanes).
Barabara iliyopo sasa itaendelea kutoa huduma kwa wale ambao hawako tayari kutumia barabara ya kulipia.
Habari njema ni kuwa, Wahandisi washauri wa michoro ya barabara hiyo tayari wameonyesha jinsi njia sita zitakavyojengwa. Kazi hii inategemewa kuanza mwaka huu, kwa mujibu wa wataalamu hao walipokuwa wakiwakilisha ripoti ya utafiti wa awali wa michoro ya barabara hiyo, New Afrika Hotel.
Barabara hii itajengwa kwa kwa utaratibu wa ubia kati ya serikali na makampuni binafsi (Public Private Partnership -PPP).

0 comments:
Post a Comment