Akizungumza katika mkutano mkuu wa
uchaguzi wa viongozi wa CWT mkoa wa mara,mwenyekiti wa chama
hicho mkoa Bw. Livingstone Gamba,amesema
agizo hilo la mkuu wa mkoa kamwe
haliwezi kutatekelezwa kwa vile
linalenga kuvuruga ratiba za vipindi vya masomo hasa wakati wa mchana wakati walimu watapolazimika kwenda nyumbani
kutafuta chakula cha mchana.
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa CWT
mkoa wa mara,amesema endapo serikali kupitia kwa mkuu wa mkoa itataka agizo hilo litekelezwe lazima wadau wote washirikishwe na kufanya maandalizi
ya kuwalipa posho za chakula kwa walimu
ikiwa ni pamoja malipo ya muda wa ziada.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa
mara Kapt.Mstaafu Aseri Msangi,ametaka
kufanyika kwa mabadiliko hayo ya muda wa
masomo kwa lengo la kuinua taalum,kuwapa
watoto muda wa mapumziko na kufufua michezo mashuleni.
0 comments:
Post a Comment