Akizunguza wakati wa
zoezi la uteketezaji wa maji hayo ambao umefanyika katika eneo la nyabange nje kidogo ya
manispaa ya musoma, meneja msaidizi
usimamiaji madeni na kodi za ndani wa TRA Bw Ernest Nkangaza,amesema kuwa maji
hayo ya aina mbalimbali kutoka nchi hiyo jirani,yameingizwa nchini kwa njia za
panya kati ya machi 9 na april 9 mwaka huu,na kusambazwa katika miji ya tarime
na Musoma.
Naye afisa afya mkoa wa
mara Bw.Bumija Mhando,amesema maji hayo kiafya si mazuri kwani yamegunduliwa kuwa ni maji ya kisima,ambayo
ukaguzi wake haufahamiki na hivyo usalama wake
unatia mashaka makubwa huku yakiwa na bei ndogo ukilinganisha na
makampuni mengini.
Zoezi hilo la
uteketezaji limefanywa na mamlaka ya mapato tanzania TRA Mkoa na idara ya
afya likisimamiwa na maafisa kutoka
jeshi la polisi na usalama wa taifa.
0 comments:
Post a Comment