Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa
sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani
Ruvuma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto)akimkabidhi Kiongozi wa
Wakimbiza Mwenge Kitaifa Juma Khatibu Chum (kulia) Mwenge wa uhuru leo
mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma
Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Mwambungu(kulia) Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa
mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto)
akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge
wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi
ulifanywa leo mjini Songea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge wa uhuru leo mjini Songea
katika Uwanja wa Majimaji ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi wa mbio za
Mwenge kwa mwaka 2015.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimezinduliwa
leo katika mkoa wa Ruvuma ambapo Rais wa Zanzibar Dkt.
Ally Mohamed Shein amewasha Mwenge huo katika uwanja wa
majimaji mjini Songea kwa ajili ya kukimbizwa nchini kote huku
akiwataka wananchi kutoruhusu makundi yawayowagawanya.
Rais wa Zanzibar Dkt Ally Mohamed
Shein akizundua mbio za Mwenge wa uhuru zilizopambwa na
burudani mbalimbali amewataka wananchi kutoruhu makundi
yanayowagawa.
Naye waziri wa habari ,utamaduni
na michezo Dkt. Fenella Mukangala anataja ujumbe wa
Mwenge wa uhuru ambapo mkimbiza Mwenge kitaifa awamu hi
ni Bw.Juma Hatibu Mchuma.
Naye mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu
anasema Mwenge utazindua,kuweka mawe ya
msingi na kukagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi
bilioni kumi mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment