Sehemu ya gharama za upasuaji huo zimetolewa na
hospitali ya rufaa BUGANDO huku wazazi wa watoto hao wakichangia shilingi laki
moja kama gharama ya vifaa, huku hospitali hiyo ikitumia zaidi ya shilingi
milioni sabini na tano kugharimia gharama za upasuaji kwa watoto hao wanaotokea
katika familia maskini zenye kipato duni. Iwapo watoto hao wangepelekwa india
kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa moyo kila mmoja angetakiwa kulipia shilingi
milioni 20.
Hawa ni madaktari bingwa pamoja na wasaidizi wao
wakiwa katika chumba cha upasuaji wa moyo cha hospitali ya rufaa bugando ambapo
ndani ya chumba hiki kazi inayoendelea ni ya kumfanyia upasuaji wa moyo mtoto
Janeth Enock mwenye umri wa miaka 10 – na kwa mujibu wa daktari bingwa wa moyo
Dk. Godwin Godfrey Shalau upasuaji huo umechukua saa 5.30 kukamilika kwa
mafanikio makubwa.
Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya rufaa Bugando Prof.
Dk. Kien Mteta anasema kwamba operesheni kubwa za moyo hapa nchini ni za
gharama kubwa, lakini kwa kutambua kuwa thamani ya maisha ya binadamu ni zaidi
ya kitu chochote, ndiyo maana hospitali hiyo licha ya kukabiliwa na changamoto ya
upungufu wa madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo, vifaa tiba na dawa pamoja na
vyumba maalumu vya upasuaji, imejitolea kufadhili gharama za upasuaji kwa
watoto hao 15 wasio na uwezo.
ITV pia imebahatika kuongea na wazazi wa watoto
waliofanikiwa kufanyiwa upasuaji huo ambapo wameelezea namna ambavyo hawakuwa
na uelewa kuhusu maradhi ya moyo yaliyokuwa yakiwasibu watoto wao.
Source :itv
0 comments:
Post a Comment